Thursday, January 12, 2017
Fahamu Kuwa Hata Wewe Ni Dereva Mzuri Tu.
Tuesday, June 28, 2016
Mambo Matano (5)Muhimu Ya Kukusaidia Katika Kukuza Biashara Yako.
Habari ya wakati huu ndugu msomaji wa
makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema
katika kupambana ili kuboresha maisha yako. Karibu tujifunze kwa pamoja mambo
matano ya kutusaidia katika kukuza biashara zetu.
Monday, May 2, 2016
Njia Za Kukufanya Ubaki Mwenye Hamasa Muda Wote.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa Makala za mtandao
huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kuhakikisha
kuwa unapambana na hatimae kujiletea matokeo bora ambayo ndiyo umekuwa ukiyapigania
kila siku, kila wakati na kila dakika. Nami nikusihi pambana bila kuchoka hata
siku maana maisha ni mapambano na wale wanaovumilia ndio hupata mema.Friday, April 15, 2016
Zifahamu Sumu Kumi(10) Zinazowatesa Vijana Kwa Sasa.
Thursday, April 14, 2016
Sababu Za Kwanini Kila Siku Wewe Hauna Muda.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa
makala za mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema
katika kubambana ili kuhakikisha kuwa unajiboresha zaidi na zaidi na baadae
unaweza kukamilisha yale ambayo umekwisha kujiwekea kama malengo katika maisha
yako. Nami nikusihi kuwa endelea kupambana pasipo kuchoka kwani harakati na
mapambano yanaendelea kila siku.
Wednesday, April 13, 2016
Zama Zimebadilika Sasa
.
Dunia inabadilika sasa, dunia inabadilika kila siku, kila
saa kila dakika, kila sekunde, kila mwaka dunia inabadilika. Je wewe
unabaadilika kulingana na dunia au unaendelea kuwa vile vile. Yaani wewe
unabaki kuwa vile vile kila siku, kila wiki, kila mwaka na kila mara au
unabadilika kulingana na wakati? Ni muhimu ukajijibu maswali haya bila
kigugumizi hata siku.
Tuesday, April 12, 2016
Tusihishie Kushabikia Tu.
Leo hii tanzania kimeibuka kitu ambacho kimeibuliwa na
serikali ya awamu ya tano. Ambacho kinatufanya wengi wetu tuwe mashabiki sana
wa hiki kitu. Wengi wetu leo hii tumekuwa tukishabikia sana sera ya mheshimiwa
raisi ya kutumbua majibu, kweli wengi sana tunashangiulia lakini leo nataka
kukusisitiza na kukuonya kuwa usiishie kuwa shabiki tu wa hii sera ya kutumbua
majipu.
Saturday, April 9, 2016
Mfahamu Mtu Huyu Vizuri.
Habari za wakati huu ndugu mpenzi msomaji wa makala za mtandao
huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema katika kuhakikisha
kuwa unapambana ilivyo ili kuweza kujiletea mafanikio, nami nasema mapambano
yanaendelea kamwe usikate tamaa hata siku moja. Maana mpambanaji huwa hakubali
kukata tamaa kirahisi.
Wakati unaendelea kupambana ili kuhakikisha kuwa
unajiletea mafanikio ni vyema ukatambua jambo hili,kwa kuwaa ninaaini kuwa wewe
hiki kitu unakifanya ndio maana nikakuuliza je? Mtu huyu unamfahamu vizuri? Najua
kila mtu anasehemu au ana mtu ambaye huwa anakuwa anamwomba ushauri sasa
kutokana na kitendo hiki ndio maana kichwa cha makala hii kinauliza mtu huyu
unamfahamu vizuri?
Wednesday, April 6, 2016
Njia Hizi Zitakusaidia Kupambana Pindi Unapokabiliwa Na Changamoto.
Maisha yamejaa changamoto za namna mbalimbali, wakati
unapambana ili kujihakikishia kuwa unapata mafanikio au matokeo mazuri juu ya
mambo fulani swala la changamoto huwa linakuwa ni jambo ambalo halihepukiki
wakati mwingine. Ni muhimu tupitie katika changamoto kwani changamoto hizi huwa
zinatujenga na kutufanya tuwe imara zaidi na zaidi maishani,
Ni muhimu kusimama imara pindi tunapokuwa tunakabiliwa na
changamoto hizo. Hii ni kutokana na sababu kuwa uwezo wa kupambana na
changamoto hizi huwa upo mikononi mwetu. Ni muhimu kutambua kuwa kwa kila
changamoto inayokukabili ni muhimu uanze kujihoji kwanza na kujiuliza wewe
mwenyewe ufanye nini juu ya changamoto husika. Kwa kufanya hivyo utajikuta
unapata majibu ambayo yanakuwa msaada mkubwa sana kwako. Pamoja na hayo
zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zaweza kukusaidia wewe katika utatuzi wa
changamoto inayokukabili:-
Tuesday, April 5, 2016
Fahamu Kuwa Kila Jambo Linatawaliwa Na Kitu Hiki
Duniani kuna vitu vingi sana ambavyo binadamu huwa
tunakuwa tunavifanya au tunataka kuvifanya, vitu hivi vinaweza kuwa vizuri au
vibaya kutoka kwa mtu mmoja mpaka mtu mwingine hii ni kutokana na tofauti za kimtazamo
miongoni mwetu binadamu. Lakini pamoja na tofauti hizi za kimtazamo huwa
tunakuwa na kitu kimoja ambacho kinaweza kutuunganisha na kutuweka pamoja na
kitu hiki ndicho ambacho wapaswa kujua na kwenda nacho kama unataka kupata
matokeo makubwa. Kitu hicho sio kingine bali ni kanuni.
Monday, April 4, 2016
Usikubali Kutawaliwa Na Vitu Hivi Viwili.
Usikubali Kutawaliwa Na Vitu Hivi Viwili.
Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za
mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika
kupambana na hatimaye kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio binafsi. Nami
nakusihi endelea kupambana mpaka kieleweke.
Wakati unaendelea kupambana ili kujiletea mafanikio basi
ni vyema ukatambua kuwa vitu hivi viwili ni hatari sana kwako endapo
utaviruhusu vikutawale maishani. Maandiko ya biblia yanatueleza kuwa “kuweni na
kiasi”. Maneno haya yana maana kubwa sana na ninaomba uyashike wewe ambae
unataka kufanikiwa. Hapa nakwenda kukushirikisha vitu viwili ambavyo kamwe
usiruhusu vikutawale maishani mwako.
Saturday, March 26, 2016
Tabia Moja Muhimu Kwako Wewe Unaetaka Kufanikiwa.
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala za mtandao
huu ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vyema mimi pia naendelea
vyema katika mapambano. Turudi katika mada yetu ya leo ambapo nataka kukushirikisha
juu ya jambo muhimu ambalo unatakiwa kuwa nalo kama kweli unataka kufanikiwa.
Jambo lenyewe ni kuhusu Kuendelea
kujifunza. Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha unajijengea tabia hii
kuanzia sasa.
Ipo nguvu kubwa sana katika kujifunza kama kweli unataka kuwa mwenye mafanikio basi
hakikisha kuwa unajifunza kila siku. Yaani usikae bila kujifunza katika kila
jambo ambalo unalifanya. Uwe mkulima, uwe daktari, uwe mwanafunzi, uwe hakimu
uwe nani wewe endelea kujifunza tu. Nakuambia hivyo kwa kuwa takwimu
zinaonyesha kuwa asilimia 40% ya watu wengi duniani huacha kujifunza pindi tu
wanapomaliza elimu zao yaa iwe sekondari au chuo, huo ndio huwa mwisho wa
kujifunza kwao. Sasa kwa wewe unayetaka kufanikiwa hakikisha kuwa haufanyi
makosa katika kujifunza.
1. Kupitia kusafiri,
unaweza kujifunza kupitia kusafiri, hii ni kutokana na sababu kuwa wanadamu
tunatofautiana kiutamaduni kwa kiasi kikubwa sana, hivyo katika kusafiri kutoka
sehemu moja kwenda kwingine kunaweza kukusaidia wewe kubadili maisha yako kwa kuwa utaweza kujifunza namna watu wanavyoishi na wanavyofanya vitu
tofauti tofauti, hivyo hii inaweza kukusaidia wewe katika kujifunza na hivyo
kubadili maisha yako. Unaweza kujifunza namna mpya ya kuendesha shughuli Fulani
kutokana na safari uliyosafiri, hii ni kutokana na sababu kuwa umebadilisha
mazingira ulikuwapo awali.
2. Kusoma vitabu,
unaweza kutafuta kitabu cha mada ambayo unaitaka vitabu vipo vingi sana swala
ni kwako wewe kuamua ni kitabu gani na kinachohusu nini unachotaka kusoma. Kuna
vitabu vya kusoma online, kuna vya kununua ambapo kampuni kama vile amazoni
zinauza vitabu vya kila namna, pia waweza kuingia google na ukasearch kitabu
unachotaka kuhusiana na mada unayotaka na hivyo basi ukapata kujifunza mengi
zaidi na zaidi.
Kusoma magazeti,
nakuona unasema magazeti dah, mbona yamejaa habari hasi, habari za kusikitisha,
habari za majonzi na simanzi na mengine mengi. Ni kweli kwa hayo unayoyasema
lakini sio kweli kuwa magazeti yamejaa mada hasi tu bali hata mada chanya zipo.
Kwenye magazeti kuna makala juu ya mambo
kama vile, afya, kilimo n.k. hivyo jambo la kufanya ni kuwa katika gazeti wewe
nunua gazeti na fuata taarifa chanya tu. Yaani fata kile ambacho unahisi
kimekufanya ununue gazeti, kama umenunua gazetiu kwa ajiri ya kusoma makala za
kilimo basi zitafute mahali zilipo kisha soma na achana na mengine.
4. Kusoma katika blog mbalimbali, hii
pia ni njia moja wapo na mabayo inakuwa kwa kasi sana ambayo wewe unayetaka
kufanikiwa unaweza kuitumia kwa kiasi kikubwa sana. Leo hii kuna blog nyingi
sana ambazo zinatoa mafunzo ya namna mbalimbali, sasa kazi ni kwako wewe kuamua
blog gani inakufaa kutokana na mada zake. Blog ni nyingi mno na zinatoa elimu
tofauti tofauti hivyo basi hakikisha kuwa unatafuta blog ya kukuwezesha wewe
kupata elimu unayota.
Maisha yanabadilika badilika kila siku
na pia utaratibu wa uzalishaji, usafirishaji na hata mawasiliano unabadilika
kila wakati hivyo ni bora uwe katika
hali ya kujifunza ili tu uwe katika nafasi nzuri ya kujifunza na hivyo kukabiliana na mabadiliko haya.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
KARIBU KATIKA DARASA HURU.
Je?
unataka kujifunza na kuwa bora zaidi?,Je? unataka usihangamie kwa kukosa
maarifa?,Je? unataka kujua namna ya kutatua matatizo na changamoto mbalimbali
zinazokukabili?,Je? unakumbana na hali ya kukata tama mara kwa mara?,Je? unashindwa
kujiwekea malengo n.k.Kama
jibu ndio basi karibu katika darasa huru. Namna ya kujiunga na darasa huru
tuma kiasi cha pesa cha shilingi 5000/=
kwa namba 0754612413 kwa mpesa (jina.
Baraka magama) au 0652612410 kwa tigo pesa. (jina: Baraka maganga). Kiasi hiki
ni kwa mwezi mmoja ambapo ukiisha utatakiwa kuchangia tena kiasi hicho hicho. Kisha,
tuma namba yako ya simu kwenda namba moja kati ya hizo huku ukiwa
umeambatanisha na jina lako kamili kama linavyojitokeza katika m-pesa au tigo
pesa. Kumbuka kufanya hivyo huku ukiwa na uhakika kuwa pesa yako imepokelewa na
hapo utaunganishwa kwenye kundi la whatsapp ambalo litakuwa na jina la DARASA HURU.
N.B, huduma hii itatolewa kwa njia ya whatsapp, hivyo
hakikisha simu yako ina uwezo wa whatsapp ndipo ujiunge ili kuepuka usumbufu.Masomo yataanza tarehe 1/4/2016. Saa tatu
kamili usiku.
Barikiwa.
Karibu sana.
Thursday, March 24, 2016
Unashindwa Kwa Sababu Kitu Hiki Kimoja Kimekushinda Kufanya.
Katika maisha tumekuwa tukifanya mambo kadha wa kadha
ambayo wakati tukifanya mambo haya huwa tunakuwa na uhakika kuwa mambo hayo ni
yenye kutulendea mafanikio makubwa maishani. Lakini kuna wakati huwa tukijikuta
tumeshindwa kufanya jambo fulani huwa tunafanya tafakari ya hali ya juu kwa
ajili ya kutaka kutambua sababu haswa iliyofanya tusiweze kufanikiwa. Baada ya kugundua sababu hapa ndipo matatizo
huanza na mara nyingi tatizo hili ndilo limekuwa likitufanya tusifanikiwe siku
zote.
Unaweza ukashindwa kutekeleza jambo fulani, na baada ya
kufanya tathimini ya nini kimekufanya usifanikiwe ukagundua pengine ni kwa
sababu uliswhindwa kutumia muda vizuri yaani kuna vitu ambavyo ulivifanya na
hatimaye vikawa chanzo cha kukupotezea muda kwa kiasi kikubwa sana na hatimaye
ukajikuta umeshindwa kulitekeleza hilo
jambo. Swala la kuwa umeshindwa kutekeleza jambo ulilolipanga kutokana na
kufanya mambo ambayo ni kinyume na uliyotakiwa kufanya ili kulitekeleza jambo fulani,
umekuja kuligundua baada ya kufanya tathimini ya kina ya nini kimekufanya
usifanikishe jambo husikia. Sasa hapa suluhu ya yote haya ni kuyaacha yaende
yale mambo yote yanayokupotezea muda lakini hapa ndipo huwa tunafanya makosa
makubwa sana maana huwa hatukubali kuyaacha yaende badala yake tunayashikilia
tu na hatimaye tunajikuta tumeshindwa zaidi na zaidi. Hivyo basi makala hii
inasema unashindwa kwa sababu umeshindwa kuyaacha yaende, hiki ndicho kitu
kimoja kinachokufanya usifanikiwe.
Ni vyema ukatambua kuwa maishani usiwe kinganganizi wa
mambo yasiyo ya msingi wala maana yoyote kwako badala yake fanya jambo moja tu
kwa yale ambayo unahisi kuwa yanakupotezea muda wako kwa kiasi kikubwa au
hayana maana maishani mwako basi yaache yaende tu hakuna namna nyingine bali ni
kuyaacha yaende tu. Usiwe mtu wa kuhaha huku na huku kuyakumbatia mambo ambayo
kimsingi hayana maana. Tumekuwa ni watu wa kushikilia mambo ambayo hayana tija
kwetu na mbaya zaidi ni kuwa huwa tunakuwa tunafahamu kabisa kuwa jambo fulani halina
tija wala maana kwangu lakini huwa tunaendelea kukomaa nayo tu au zaidi na
zaidi yaani tunakomaa nayo tu. Sasa jambo hili ndilo linatufanya tuzidi
kushindwa kila mara maishani.
Nyani ni kiumbe ambaye kwa wakati mwingine huonekana ni
mjanja sana na ni msumbufu kwa wanadamu, hili kwa wale ambao wanafanya shughuli
za kilimo katika maeneo ambayo nyani ni wengi watakuwa wananielewa kirahisi
sana, lakini nyani huyu huyu ambaye huonekana mjanja huwa anaponzwa na tabia
moja tu nayo ni ile ya kuto kuacha yaende. Kule nchini Brazili wanaowinda nyani
hutumia njia rahisi sana ya kumtega nyani, wao huchukua mtego ambao huwa na
uwazi sehemu moja ambapo nyani anaweza kupitisha mkono wake, kisha katika lile
tundu huwa wanatumbukiza ndizi na kisha kuweka ule mtego pahali fulani. Sasa nyani
akija huwa anataka kuchukua ile ndizi, lakini kwa jinsi ambavyo mtego ule
ulivyo ni kuwa nyani akishaingiza mkono wake hawezi kutoka akiwa ameshikilia
ndizi, nyani hulitambua hilo kuwa hawezi kutoa mkono akiwa na ndizi hivyo aidha
aiachie ndizi ili asikamatwe au la. Lakini cha ajabu ni kuwa nyani huyu
huendelea kung’ang’ania ndizi husika mpaka wenye mtego hufikia na kuweza
kumkamata. Hivyo kinachomponza nyani siku zote ni ile tabia ya kuto acha
yaende.
Sasa tabia hii ya nyani ndio hata binadamu tumekuwa nayo
mtu utakuta anayafahamu fika madhara ya utumiaji wa pombe kupita kiasi lakini
anaendelea, madhara ya uvivu lakini anaendelea, madhara ya kutokuweka malengo
lakini anaendelea tu kufanya mambo ambayo yanamfanya asiweke malengo n.k.
Tambua kuwa uwezo wa kushindwa au kushindwa upo mikononi
mwako chagua leo kushinda na utashinda tu na chagua leo kutokushinda na
hutoshinda kamwe vilevile.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
:-barua pepe
-Bmaganga22@gmail.com
Wednesday, March 23, 2016
Hii Ndio Siri Ya Kushinda Maishani.
Ni wengi sana tumekuwa tukitaka kushinda maishani yaani
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Ni kweli kila mpambanaji huwa anataka kushinda
katika kila pambano analoshiriki na ndio maana kiuhalisia kila binadamu
anapenda kufanikiwa na ndio maana kichwa cha makala nimeamua kukiita siri ya
kushinda maishani nikiwa nataka kulenga siri ya kufanikiwa maishani.
Tumekuwa ni watu wenye kutaka kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa kila mtu anapenda apate mafanikio makubwa, mimi nataka mafanikio, wewe
unataka mafanikio na yule anataka mafanikio. Lakini kwanini tumekuwa tukijikuta
kila mara tuko pale pale tulipokuwa jana yaani hatuendi mbele hata hatua moja
kimaisha. Kila mara tumekuwa watu wa kushindwa hata kama tukijitahidi kupanga
mipango muhimu na mizuri lakini wapi huwa tunajikuta tumeshindwa tena na tena.
Je unakumbwa na tatizo hili la kushindwa mara kwa mara
pamoja na kwamba umejiwekea malengo, umepanga mikakati ya kutekeleza malengo
yako na mengine mengi? Kama jibu ndio karibu nikupe njia rahisi ya kuweza
kuepukana na hiyo hali.
Siri ya kushinda ni vitendo.
Hii ndio siri kubwa na ambayo ninata uifahamu kwanzia leo kuwa siri ya kushinda
ni vitendo. Kwanini nimesema hivyo, nimesema hivyo ni kwa kuwa takwimu
zinaonyesha kuwa watu wengi sana wamekuwa au tumekuwa ni mabingwa wa kupanga
mipango mizuri, kuweka mikakati kabambe, kuweka malengo mazuri sana ambayo
ukiyasoma kwa kiasi kikubwa ni yanavutia sana tena sana, kiasi kwamba kila
ukiyasoma yanakuvutia na unayafurahia lakini wakati unafanya hivyo unasahau
kitu kimoja kwamba mipango tunayoiweka sio kwa ajili ya kuiweka kwenye
makaratasi au kwenye karatasi tu bali tunatakiwa kuifanyia kazi yaani tuweke
katika vitendo.
Kila kitu huanza kwa mpango, malengo na mikakati ambayo
mara nyingi sana huwa inakuwa imeandikwa kwenye karatasi, wengi tunaweza
kufanya hili jambo lakini jambo ambalo linatushinda ni kuhamisha yale yaliyomo
katika makaratasi au karatasi na kuyapeleka katika vitendo, hili ndio jambo
ambalo linatushinda kwa kiasi kikubwa sana na ndio maana tunashindwa kushinda (kufanikiwa).
Kama sio mtu wa kuchukua hatua ya kutenda kamwe sahau
kuhusu kushinda maana huto weza kushinda kamwe maishani, kushinda huja kutokana
na kuamua kuweka ile mipango tuliyojiwekea katika vindeo hivyo basi siri ya kushinda
ni vitendo. Unatakiwa kutenda na uendelee kutenda bila kuchoka, kuhairisha wala
kukata tamaa maana katika matendo ndimo huwa tunapata ushindi.
Mara nyingi tumekuwa tunashindwa kuchukua hatua ya
kutenda kutokana na sababu mbalimbali kama vile:-
1. Kuhisi
uvivu pale tunapotaka kutenda, kama unakabiliwa na hii
hali basi jua kabisa hiyo hali sio nzuri kwako na inaweza kukuzuia wewe kutenda
jambo. Hivyo tambua kuwa hakuna matunda mazuri katika uvivu, yaani uvivu hauzai
matunda mazuri hata siku bali huzaa matunda mabovu hivyo uogope uvivu.
2. Uoga, wakati mwingine
pale unapotaka kuchukua hatua ya kutenda unakabiriwa na hali ya kuogopa kuwa
watanichukuliaje au ntaonekanaje hali hii inaweza kukufanya usichukue hatua
yoyote na hivyo kujikuta umeshindwa kutenda na hatimaye unabaki pale pale.
3. Hofu, wakati mwingine huwa
unakumbwa na hofu pale unapotaka kutenda jambo fulani. Hofu ya kushindwa, hofu
ya kuto kujulikana ni mifano wa hofu ambazo zinaweza kukuzuia wewe kuto tenda
jambo fulani. Kabiliana na hofu hizi mara moja.
Hakika siri ya mafanikio/ kushinda ni
vitendo, kuweka malengo sio mafanikio ila kuyaweka malengo yako katika matendo
ndiko huleta mafanikio, kupanga mikakati, na mipango pia hakuleti mafanikio ila
kutenda. Hiyo ndio siri niliyopanga kukushirikisha leo hii, natumaini utakwenda
kushinda sasa.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
:-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.
Mambo Matatu Yanayoweza Kukufanya Usitimize Ndoto Yako.
Kila mtu ana ndoto zake maishani hilo ni swala ambalo
naliamini maishani kuwa wewe una ndoto, yule anandoto zake na mimi ninazo za
kwangu ambazo kwa kiasi kikubwa sana zinatofautiana sana tena sana. Kwa kuwa
ndoto zetu zinatofautia hili ni jambo jema maana hili ndilo hupelekea hata sisi
kutofautiana kimaisha na kimatendo. Hivyo sio jambo baya kuwa na tofauti ya
ndoto kati yangu mimi na wewe na yule.
Leo nataka nikushirikishe mambo matatu ambayo yanaweza
kukufanya ushindwe kutimiza ndoto zako mambo hayo ni kama yafuhatayo.
Hofu, ile hali ya kuwa na
wasiwasi mwingi juu ya lile unalotaka kulifanya inaweza kuwa adui mkubwa sana
wa ndoto zako. Najua kuwa unazifahamu aina nyingi sana za hofu, lakini mimi
nataka kugusia hofu ya aina moja tu ambayo ni hofu ya kuto kujulikana. Mara ngapi
umekuwa kila unapotaka kufanya jambo fulani unasikia ndani yako kuna sauti
inakuhamaasisha kuwa nani anakujua wewe hapa mjini nani?, ukisikia sauti hiyo
usijidanganye kusema ni malaika wa mungu anakusihi uache, hapana jua hiyo ni
hofu. Ni kweli hakuna anayekujua lakini hilo halikuzui wewe kuweza kutekeleza
jambo fulani. Kweli hawakujui kwa sababu hujajitambulisha kwao wewe ni nani. Sasa
pengine kupitia lile unalotaka kulifanya
ndilo linaloweza kukufanya ufanikiwe kwa kiasi kikubwa na hatimaye ukawa
umejitambulisha kuwa wewe ni nani na ukawa usha fahamikia tayari. Sasa kabiliana
na hii hofu tenda lile unaloliona ni sahihi na utajulikana tu. Hakuna aliyezaliwa
akiwa anajulikana.
2. Kutaka kuanza na makubwa,umekuwa
ni mtu wa kutaka kusubiri eti mpaka uwe na kitu kikubwa ndio uweze kutenda
jambo fulani. Ndugu msomaji waswahili walisema “haba na haba hujaza kibaba”. Anza
na kidogo wala hata usiogope kuanza na kitu kidogo maana kidogo huzaa kikubwa
sasa wewe unaposubiri eti upate kikubwa ndipo utende huko ni kujidanganya na
kujipotezea muda na kuendelea kudumaza ndoto yako maana hakuna namna ambayo
unaweza kupata kitu kikubwa bila kupitia
kitu kidogo hivyo basi njia ya uhakika ya kukufanya wewe uweze kufanikisha
ndoto zako ni kuanza na kidogo siku zote. Hata kama ni biashara unataka kuwa na
biashara kubwa sana wewe anza na mtaji hata wa milioni mbili hata kama ndoto
yako ni kuwa na biashara ya milioni ishirini na hiyo milioni mbili baada ya
muda itajizalisha na kufikia hizo milioni ishirini unazozitaka. Hivyo nakusii
usiue ndoto yako kwa kutaka eti kuanza na kikubwa maishani bali wewe anza tu
pale unapohisi upo tayari na unachakuanzia hata kama ni kidogo.
3. Kuto kuwa na maono sahihi,
kama unataka kufanikiwa lazima uwe na maono. Maaono ni ile hali ambayo unaweza
kuwa unajionea mambo ya mbele kifikira zaidi. Mfano unajionaje wewe baada ya
miaka mitano toka leo. Kila mtu ana namna ambayo anajiona atakavyokuwa baaada
ya miaka mitano mwingine anaweza kujiona kuwa anakuwa mtu maarufu sana, anakuwa
mfanyakazi bora, mjasiriamali mkubwa n.k. hayo ndio maono. Sasa ikitokea huna
uwezo wa kuona ndani ya miaka mitano utakuaje basi hii ni njia moja wapo ya
kuweza kuua ndoto zako. Maono huwa kama tasirwa/picha mabayo unayaona maisha
yako kifikira zaidi. Na maono sio malengo hivyo usijichanganye niliposema labda
unajiona kuwa mfanyakazi bora baada ya miaka mitano ukajua ni malengo hapana
malengo na maono vinatofautiana. Ingawa maono yanategemea malengo yako na
malengo yako yanategemea maono yako. Hivyo basi hakikisha una maono sahihi
yaani unauwezo wa kujiona ndani ya miaka mitano utakuaje au utakuwa wapi
kimaisha.
Mwandishi: Baraka Maganga.
Mawasiliano:-simu-0754612413/0652612410.
:-barua pepe -Bmaganga22@gmail.com.
Monday, March 21, 2016
Jambo Hili Halitakusaidia Lolote Maishani.
Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za mtandao huu, ni matumaini yangu
kuwa hu mzima na unandelea vizuri katika kupambana zaidi na zaidi ili tu
kuhakikisha kuwa unajiletea mafanikio ambayo umeyakusudia maishani. Nami nasema
vizuri na endelea kupambana zaidi na zaidi bila kuchoka kwani mafanikio ndio
kila kitu ambacho mtu anakitaka maishani hivyo ni haki yako wewe kupambana ili
kuhakikisha unayapata mafanikio.
Ni wengi sana ambao tumekuwa tukipigana kwa hali na mali katika kuhakikisha kuwa tunajiletea mafanikio, hili ni jambo ambalo huwa tunalifanya wengi wetu na tumekuwa tukilifanya kwa muda mrefu. Ni vizuri sana kufanya hivyo binafsi huwa nafarijika sana napowakuta vijana wenzangu wanazungumzia mafanikio na wanapambana ili kujiletea mafanikio kama unafanya hivyo naomba pokea pongezi zangu. Hongera hongera sana.
Leo nataka kuzungumzia swala moja ambalo linaweza
kukufanya usifanikiwe na ndio maana kichwa cha makala hii kinasema jambo hili
halitakusaidia lolote. Jambo lenyewe ni kuwa na mtazamo hasi juu ya watu
waliofanikiwa. Nimeamua kulizungumzia hili kwa kuwa kumekuwa na baadhi ya watu
ambao wamekuwa na mtazamo mbovu juu ya watu waliofanikiwa mfano wanawachukia
watu waliofanikiwa, wanawaona kama ni watu wachoyo, wabinafsi, walaghai,
wanyanyasaji na wenye tamaa za pesa kuliko watu wengine.
Pengine unasababu zako za kukufanya uwachukulie watu
wenye mafanikio kwa namna ambayo unawachukulia hivi sasa, lakini naomba
nikuambia haya kuwa kwanza pole sana kwa kuwatazama watu waliofanikiwa katika
mtazamo hasi, pili naomba nikuambie kuwa siujali ukubwa wala udogo wa sababu
inayokufanya wewe kuwachukia watu waliofanikiwa ila nachotaka kukuambia ni kuwa
unachofanya sio sahihi. Sio sahihi kwa sababu haupaswi kufanya hivyo badala
yake unatakiwa kuwachukulia watu walio fanikiwa kama darasa na waalimu wako.
Hakika kama unataka kufanikiwa hakikisha kuwa unajenga
uhusiano mzuri na walio fanikiwa na kubwa jenga mtazamo chanya juu yao. Waone kuwa
ni kama watu ambao ndio nyenzo muhimu ambazo unaweza kuzitumia na ukafanikisha
mambo yako kwa kiasi kikubwa. Ukiwachukia watu wenye mafanikio ni dhahiri kuwa
hata mafanikio nayo utayachukia, japo unaweza kujifariji kuwa mi nawachukia tu
wenye mafanikio ila mafanikio nayapenda huko ni kujidanganya kwa hali ya juu
yaani unahisi upo sahihi kwa mwonekano wa nje lakini ndani yake umejiharibia
kila kitu.
Wachukulie watu wenye mafanikio kama darasa kwako, wachukulie
kama watu ambao unaweza kuwa tumia kama daraja la kuweza kukuvusha wewe toka
hapo ulipo na kukupeleka kule unako kutaka. Ukiwa na mtazamo chanya juu ya watu
wenye mafanikio hii itakusaidia wewe
kuweza kuwafuata na kuweza kujifunza mambo mengi kutoka kwao tena kwa kiasi
kikubwa.
Jambo la msingi ambalo unatakiwa ulijue kuanzia sasa na
ulifahamu kwa asilimia zote ni kuwa mafanikio huja kwa kujifunza kutoka kwa
walio fanikiwa sasa kama unawachukia watu wenye mafanikio hii inamaanisha nini,
hii inamaanisha kuwa hutoweza kujifunza kutoka kwao, na kama ukishindwa
kujifunza kutoka kwao maana yake utajifunza kutoka kwa walioshindwa na kama
ukijufunza kutoka kwa walioshindwa basi na wewe utashindwa tu.
Hakuna sababu ya kuwachukia waliofanikiwa bali jambo ambalo
wewe unatakiwa kufanya ni kuwapenda na kutaka kujifunza zaidi kutoka kwao, hii
ndio njia ambayo inaweza kukufanya wewe kuwa mwenye mafanikio makubwa kama wao.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga
Waweza wasiliana nami kwa nambari za simu
0754-61-24-13 au 0652-61-24-10.
Au kwa barua pepe
Bmaganga22@gmail.com
Wednesday, February 24, 2016
Yatathimini Matumizi Yako Ya Pesa Kwa Umakini Kabla Hujasema Tatizo Mtaji
Habari za wakati huu ndugu mpendwa msomaji wa makala za mtandao
huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri sana katika
kutekeleza majukumu yako ya hapa na pale, ni muhimu uendelee kufanya hivyo kwani
mapambano yanaendelea kwa kiasi kikubwa sana hivyo jambo la msingi ni
kuyaendeleza mapambano hayo kwa kasi ya ajabu ili kuweza kuyatekeleza yale
ambayo ni ya msingi na ambayo kwa upande mwingine ndiyo tumekuwa tukiyataka
maishani.
Wakati ukiendelea kupambana ndugu mpendwa msomaji wa
makala hii hebu kwa dakika moja tu fikiria juu ya matumizi yako. Naposema
matumizi najua nakuwa na eleweka kwa kiasi kikubwa tu, matumizi nayo
yazungumzia hapa ni matumizi ya pesa. Nilipenda kichwa cha makala ya leo kiwe
mtaji sio tatizo lakini nimeamua kukiweka
kama kilivyo kwa kuwa ntakacholenga kukisema kitakuwa na uhusiano tu na
mtaji. Tumekuwa ni watu wa kulalamika sana juu ya mitaji, sana tena sana.
Lakini leo hii naomba tujadili na tuweze kuelewana kuwa mtaji sio tatizo bali
ni vichwa vyetu ndivyo vyenye matatizo. Hapa leo naongea na wafanyakazi uwe
mfanyakazi wa serikali au shirika binafsi naongea na wewe hapa leo.
Kwanini nataka niongee na wafanyakazi kwa kiasi kikubwa
ni kwa sababu ya vituko vya wafanyakazi, kila mtu leo hii anaamini kuwa
wafanyakazi mishahara yao haiwatoshi kwa kuwa wao ni walalamikaji wakubwa kuwa
mishahara haiwatoshi. Lakini mimi nataka kusema kuwa mishahara inawatosha.
Tutoke huko maana sio lengo la makala. Lengo la makala ni kutaka kuonyesha kuwa
mtaji sio tatizo kwa kupitia kuchunguza matumizi yetu ya pesa tunazozipata kama
mshahara wa shughuli zetu.
Wakati nikiwa kidato cha sita miaka michache huko nyuma
nilijifunza kutoka katika kitabu cha
rich dad poor dad cha bw. Kiyosaki tofauti kati ya asset na
liabilities. Kwa mujibu wa kiyosaki
anafafanua assets kama kitu ambacho kinachoingiza pesa mfukoni ili hali
liabilities ni kitu ambacho kinatoa pesa mfukoni. Hapo hapo rudi katika kichwa
cha makala, tathimini matumizi ya pesa zako, wewe pesa zako unazitumia katika
nini, je ni asset au liabilities? Jijibu mwenyewe. Kiyosaki aliendelea kusema
kama unataka kuwa tajiri nunua assets na kama unataka kuwa masikini nunua
liabilities. Hapo hapo turudi kwako huwa unanunua nini?. Rudi nyuma tena
jiulize kwanini mpaka leo hauna mtaji wa kuanza biashara au jambo jingine
tofauti na kazi yako hiyo. Tatizo mtajii eehe wenzio waliupataje huo mtaji sasa?.
Aya nakuambia hivi tatizo sio mtaji tatizo ni akili yako hiyo. Kama unataka
kujua kama mshaara wako unaweza kukupatia mtaji chunguza matumizi yako ya pesa.
Unatumia pesa nyingi sana kwenye liabilities ndio maana hauna mtaji. Kama
unabisha sawa ila huo ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli.
Wafanyakazi wengi wanamtindo wa kununua vikolokolo ndio
maana hawapati mitaji, . naposema vikolokolo namaanisha kuwa vitu visivyo na
tija wala umuhimu bali katika hali ya kutaka kuuridhisha moyo, mwili au wenzio.
wewe huyo kila aina ya simu unataka uwe nayo, baba/mama utaweza kushindana wa
wachina kila siku wako na matoleo mapya. Kila uzinduzi wa albamu unataka uende,
kila tamasha la muziki wewe humo, kila fashioni mpya ya nguo humo, kila mkopo
unataka ukope alafu mkopo huo unataka ukanunue pikipiki ya kuendea kazini.
Pikipiki itakudai mafuta alafu utajikuta huna pesa. Kwa matuzimi ya namna hii
kweli mshahara haukutoshi na hauwezi kupata mtaji. Lakini ukipunguza mfano
ukawa na simu hata teckno p5 inatosha mbona nayo utaingia fb, whatsapp na
instrgram, pia makala zangu utasoma sasa yanini bwebwe nyingi za masimu kibao.
Ni muhimu kupendeza kimavazi lakini sio muhimu kuwa na
kila aina ya vazi. Ni muhimu kuwa na pikipiki lakini ujue ni assets au
liabilites. Ni muhimu kuuzulia matamasha na uzinduzi wa albamu za wasanii
uwapendao lakini sio wote. Jiulize kama kwa mwezi unatumia shilingi laki mbili
kutoka katika mshahara wako katika liabilities, ukiachana nazo mara mwaka
utakuwa hujapata mtaji wewe au unaleta habari gani hapa. Chemsha kichwa sio
kulalama tu. Think beyond.
Uwezo wa kupata mtaji kupitia mishahara yetu tunayo sema
shida ni akili zetu na vichwa vyetu. Unakopa mkopo unanunua jiko la gesi, sijui
sofa, sijui sabufa usiposikiliza mziki utakufa simu yako haina mziki? Kuwa na
nidhamu na pesa vinginevyo utaishia kulalamika mpaka siku yesu anarudi.
“If you want to be rich buy
assets” ROBERT KIYOSAKI.
“Mtaji sio tatizo tatizo ni
vichwa vyetu”.
Je unataka kujipatia kitabu
cha Robert kiyosaki ili kujifunza zaidi na zaidi usiwe na shaka.nitumie email
kupitia email yangu ya hapo chini na neno, “nataka kitabu cha rich
dad poor
dad” nami ntakutumia.
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.
Tuesday, February 23, 2016
Utavuna Ulichopanda Na Huto Vuna Usichopanda.
Habari za wakati huu ndugu mpenzi msomaji wa makala za
mtandao huu, mtandao ambao umelenga kukupatia maarifa ambayo ukiyatumia huta
kaa ujute kwanini uliamua kujiunga na mtandao huu ili uwe unasoma makala zake.
Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri sana katika mapambano nami nasema
mapambano yanaendelea na yataendelea.
Ukipanda mahindi utavuna
mahindi.
Ukipanda mtama utavuna mtama
Ukipanda matikiti utavuna
matikiti.
Usipopanda maharage hutovuna
vuna maharage.
Usipopanda mti hutovuna mti.
Usipopanda alizeti hutovuna
alizeti.
Nimeweka kauli hizo hapo juu lengo sio kukuchosha au
kukutaka uzisome tu na kuishia kuzishangaa hapana lengo la kuziweka kauli hizo
hapo juu ni kutaka uweze kunielewa toka mwako ambacho nakimaanisha maana hapa
nataka tuelewane kiurahisi zaidi pengine kuliko siku zote ndugu msomaji wa
makala hii. Kama kichwa kisemavyo kuwa utavuna ulichopanda na hutovuna
usichokipanda. Hivi nikikuuliza ndugu msomaji wa makala hii kuwa uonapo kauli
hii unajifikiria nini juu ya maisha yako. Yaani unaonaje juu ya matokeo
uyapatayo kutokana na shughuli zako?. Na uionapo kauli hii unahusianisha vipi
na ulalamishi au ulalamikaji wa watanzania wa leo. Binafsi naamini kuwa kama
watanzania tungekuwa wenye kuielewa kauli hii vizuri basi leo hii kusingalikuwa
na mtanzania anayekaa na kuanza kuilaumu serikali, wazazi, ndugu au walezi wake
kuwa wao ndio chanzo cha yeye kuto kufanikiwa. Kwanini nasema hivyo mimi nasema
hivyo kutokana na kauli ilivyo.
Kauli inasema utavuna ulichopanda. Kwahiyo ukipanda
ulalamishi utavuna ulalamishi kwahiyo ni kuwa ukimlaumu mtu nae atakulaumu au
nawewe utalaumiwa na wengine. Kauli inasema utavuna ulichopanda na hautovuna
usichopanda hakuna sehemu ambayo imesema utavuna ulichopandiwa na hautovuna
ulichopandiwa hapa naweza kusema kauli hii haitambui jambo linaloitwa utegemezi
hivyo basi kama vijana wangekuwa wanaielewa vyema kauli hii wangeacha maswala
ya kuwategemea wazazi wao kwa kila kitu badala yake wangeanza kupanda mbegu Fulani
ambazo zingeweza kuwazalia matunda Fulani ambayo kwa siku za baadae
zingewaletea matokeo mazuri.
Kauli hii pia inatukumbusha juu ya uwajibikaji nikiisoma
kauli hii nakumbuka juu ya uwajibikaji kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa
mafanikio yake na sio kumtegemea mtu akuletee mafanikio. Huwa tunakwepa
majukumu yetu kwa kiasi kikubwa sana, sasa kauli hii inatukumbusha juu ya
uwajibikaji juu ya maisha yetu. Utavuna ulichopanda maana yake unahusikia moja
kwa moja juu ya matokeo uyapatayo maishani. Kama wewe ni masikini mpaka sasa
tambua kuwa umepanda mbegu za umasikini na ndio maana uko masikini mpaka leo.
Hakuna mtu anayehusika na umasikini wako bali ni wewe mwenyewe ndiye
unayehusika nao maana ni mbegu ambazo umepanda wewe mwenyewe bila kumhusisha
mtu mwingine hivyo basi unawajibika kwa umasikini wako na sio vinginevyo.
Kauli hii inanikumbusha juu ya ubora wa mbegu zetu yaani
kama unataka kupata matokeo bora ni
wakati sasa wa kupanda mbegu bora, maana si utavuna ulichopanda maana yake ni
kuwa mbegu bora huzaa mbegu bora na
mbaya huzaa mbaya nyenziye. Hivyo basi panda mbegu bora maana ndiyo ikufahayo.
Maishani tumekuwa tukikumbwa na mambo mengi sana na
tumekuwa watu wa kuwasakizia wengine kuwa ndio wahusika wa mambo hayo
yanayotutokea hata kama ni kwa kuwasingizia lakini huwa tunataka kuuaminisha
umma kuwa hali zetu mbaya ni matokeo ya watu au vitu fulani kumbe tunakuwa
tunajidanganya sasa jambo la msingi hapa ni kuwa kwa kuwa umegundua kuwa
utavuna ulichopanda hata ikitokea watu wanakushawishi uanze kulalamika juu ya jambo
fulani we achana nao maana ukweli wa mambo ushaujua.
Uvivu huzaa uvivu.
Lawama huzaa lawama.
Visingizio huzaa vizingizio.
Tamaa huzaa tamaa.n.k
Ni mimi rafiki yako,
Baraka Maganga.
Wasiliana nami kwa nambari za simu 0754612413/0654612410 au kwa barua pepe:- Bmaganga22@gmail.com.
Monday, February 22, 2016
Fanya Kitu Hiki Na Utafanikiwa Tu
Tuesday, February 16, 2016
Usifanye Kwa Kuwa Umeona Wanafanya.
Subscribe to:
Posts (Atom)












